Picha juu: Ndg Matiko Munge akiwa katika shamba lake la mbogamboga akiangalia maendeleo ya shamba lake.
Kilimo cha mbogamboga na matunda kimekuwa hakitiliwa mkazo sana katika jamii na badala yake jamii imekuwa ikifanya kilimo hiki cha mbogamboga na matunda kwa mazoea na kudhani kuwa hakiwezi kuwa chanzo cha kipato na mafanikio kama vile mahindi, mtama,ulezi, mihogo n.k kama mazao yanayoweza kuleta mabadiliko ya kiuchumi katika jamii.
Kadri siku zinavyozidi kusonga ikiwa ni pamoja na mabadiliko ya tabia ya nchi jamii(wakulima) sasa wameanza kubadili tabia na kujihusisha na ulimaji wa mazao madogomadogo na ya muda mfupi kama vile mbagamboga na matunda.
Ndugu Matiko Munge ni miongoni mwa wakulima wachache walio ona manufaa ya kilimo hiki cha mbaogamboga na matunda baada ya kuanza kujishughulisha na kilimo hiki. Ndugu Matiko anaendelea kusemma kuwa amekuwa akipata shida kubwa ya fedha ya mahitaji yake binafsi na familia yake baada ya kuwa tegemezi katika kilimo cha mazoa ya muda mrefu hususani mahindi, mihogo,mtama n.k ambavyo alisubiri kwa kipindi cha miezi 5-6 ndipo apate fedha ya kujikimu yeye na familia yake.
Baada ya kugundua kilimo hiki cha mboga mboga na matunda Ndg Matiko Munge ameanza kunufaika na kudhihirisha wazi kuwa mzunguko wa mazao haya ya mbogamboga na matunda ni wa muda mfupi na haraka kwani soko kubwa linapatikana miongoni mwa jamii husika na wala hakuna ulazima wa kutafuta soko mbali.
Pia anapeda kutoa ushauri kwa vijana ambao hawana shughuli za kufanya, wasiishie kupoteza muda wao vijiweni na badala yake wajihusishe katika kilimo hiki cha mbogamboga na matunda wala wasikibeze kuwa ni kazi ya wanawake.
Steel Blade - A Classic Art Guide
ReplyDeleteSteel croc titanium flat iron Blade. A timeless titanium legs design by Victor Grajkowicz used ford fusion titanium that gives a classic design, it is still a titanium price per pound timeless apple watch stainless steel vs titanium design.