SHUGHULI ZA UVAMIZI KATIKA MGODI WA ACACIA NORTH MARA ZA KUTAFUTA MAWE YA DHAHABU ZIMEKUWA KERO KWA BAADHI YA VIJANA NA KUAMUA KUJIAJIRI BAADA YA KUPATA USHAURI KUTOKA SHIRIKA LA TAECA.




H:\DCIM\132___08\IMG_4770.JPG
Mgodi wa  ACACIA North Mara, ni Mgodi unaozungukwa na vijiji saba ambavyo ni Nyamwaga, Genkuru, Nyakunguru, kewanja, Nyangoto , Matongo na Kerende.Changamoto kubwa iliyopo katika maeneo haya ni vijana wengi wa vijiji jirani kukosa ajira na kutojishughulisha katika shughuli za uzalishaji mali, hali ambayo imepelekea kujiingiza katika swala la uvamizi wa kutafuta mawe ya dhahabu (intruder) katika mgodi wa ACACIA North Mara, shughuli ambayo wengi wao wanakiri kuwa ni Ngumu na ni hatarishi katika maisha yao na ni ya kubahatisha, hali ambayo vijana wengi wamejikuta wakipata hali ngumu kiuchumi kadri siku zinavyokwenda kwa sababu ya kutokuwa na uhakika wa kupata kipato katika shughuli  hiyo.
Ndg Kiluka ni miongoni mwa vijana walioathiriwa kiuchumi baada ya kujihusisha na shughuli ya uvamizi wa mgodi na kujikuta akipoteza muda mwingi bila mafanikio yoyote na sasa ameamua kujiajiri katika shughuli ya ufyatuaji tofali ambapo sasa anaanza kuona mabadiliko  ya kiuchumi tofauti na alivyokuwa akivamia mgodi wa ACACIA North Mara ulioko Nyamongo.

Pia anamaliza kwa kuwashauri vijana wenzake kutopoteza muda na badala yake wajiajiri katika shughuli nyingine za uzalishaji mali tofauti  na shughuli ya uvamizi japo mafanikio yatachukua muda mrefu na ameiomba serikali ipange mikakati ya kuwasaidia vijana kimtaji ili waweze kujiajiri wenyewe.

About TAECA.TZ

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment