VIJANA NA UJASIRIAMALI.
Ujana ni kipindi muhimu sana kwa maendelea katika maisha ya binadamu. Watu waliotumia ujana wao vizuri, ndio walio fanikiwa kimaisha, na waliotumia ujana wao kwa anasa na kutojishughulisha ndio waliopoteza dira ya maisha na kupata wakati mgumu sana katika uzee wao.
Ndg Kebe Wambura Maganda ni kijana mwenye umri wa miaka 26, mkazi wa kijiji cha Nyamwaga aliutambua wajibu wake kama kijana akiwa na umri wa miaka 19 baada ya wakati mgumu alio kutana nao alipo maliza elimu ya shule ya msingi na kukimbilia mjini kwa ajili ya kutafuta kazi, lakini aligundua kuwa hakuwa amefanya maamuzi sahihi hapo mwanzo ya yeye kwenda mjini kutafuta maisha mazuri, ndipo alipo chukua tena uamuzi wa kurudi kijijini na kujiajiri katika shughuli za kilimo na ufyatuaji wa tofali.
Baada ya hapo Ndg Kebe aliona mabadiliko makubwa ya kimaendeleo katika maisha yake, maana amenunua uwanja na kujenga nyumba na sasa anaishi nyumbani kwake na familia yake na pia anafuga Ng’ombe, mbali na hapo Kebe ameweza kununua viwanja vya ardhi visivyo pungua sita(6) na baadhi ya viwanja hivyo amepanda miti kwa faida yake ya baadae na watoto wake.
“Anaendelea kusema , hata kijijini inawezekana endapo kijana atachukua hatua za kujishughulisha kwa bidii katika shughuli zenye tija na ambazo hazivunji sheria na taratibu za nchi”. Anamaliza kwa kusema “ kukata tamaa na kutothubutu ndicho chanzo kikubwa cha vijana wengi kutojishughulisha na kujikuta katika wakati mgumu sana katika maisha.
Kijana Acha Kulala FUMBUKA
ReplyDelete