Shirika la Tarime Agricultural and Environmental conservation
Association (TAECA) ni shirika lisilo la kiserikali (NGO) lililoanzishwa
mwaka 2014 na kupata usajili kamili tarehe 14 mwezi 04 mwaka 2015. na
kupewa namba ya usajili 00NGO/0007915.
Lengo
kuu la shirika ni kuunganisha Nguvu ya pamoja katika kutoa elimu juu ya
kanuni bora za kilimo, ufugaji, Elimu jamiii na ujasirialimali kwa lengo
la kuinua uchumi katika jamii ya kitanzania.
Eneo
la utendaji kazi la shirika la TAECA ni katika eneo lote la Tanzania
Brara na ofisi ndogo zitafunguliwa kila sehemu ambapo shirika litakuwa
na mradi.
DIRA YA SHIRIKA (VISION)
Kuwa
na jamii inayoendesha shughuli za kilimo/ufugaji endelevu kwa kufuata
misingi bora ya kilimo na ufugaji kwa lengo la kukuza uchumi wa kizazi
cha sasa na kijacho.
DHAMIRA YA SHIRIKA (MISSION)
Kuiwezesha
jamii, sekta binafsi na wadau wengine kushiriki katika kuinua kilimo,
ufugaji na utunzaji wa mazingira kwa kutumia mbinu shirikishi jamii ili
kuleta tija na uchumi imara katika jamii ifikapo mwaka 2050.
0 comments :
Post a Comment