Wafugaji wengi wa Nyuki hufikiria kuwa faida ya Nyuki ni uzalishaji wa Asali tu, lakini kuna mazao mengine zaidi ya asali yatokanayo na Nyuki.
Nta ni moja ya zao litokanalo na Nyuki, Nta hutengenezwa na nyuki wachanga ambao hutoa ute uliochanganyikana na vitu vingine ili kutengeneza masega ya Nyuki. Masega yanapo yeyushwa na kuchujwa, Nta hubaki na binadamu huitumia kwa shughuli mbalimbali kama vile kutengeneza mishumaa, vipodozi vya wanawake, kuimarisha nyuzi za nguo viwandani n.k.
Kikundi cha ufugaji Nyuki Nyarero ni moja ya wafugaji waliokuwa wakidhani kuwa nyuki huzalisha Asali tu na si vinginevyo, lakini baada ya kuhudhuria semina ya mafunzo ya namna ya kuvuna mazao yatokanayo na nyuki iliyokuwa imeandaliwa na shirika la TAECA, wamefanikiwa kuvuna zao la pili tofauti na Asali mbalo ni Nta.
Kikundi cha ufugaji Nyuki Nyarero, wao hawapo tayari kuuza zao la Nta bali wamemwomba mlezi wao Ndg Joseph Benard Muhenga kuwawezesha kupata mafunzo ya namna ya kutengeneza mishumaa ili waweze kuongeza thamani ya zao hili la Nta na kunufaika mara dufu.
0 comments :
Post a Comment