ELIMU KWA UMMA JUU YA HIFADHI YA MAZINGIRA INAHITAJIKA KATIKA JAMII ZINAZOISHI NA KUJISHUGULISHA PEMBEZONI MWA MILIMA YA ASILI ILI KUEPUKA UALIBIFU UNAOJITOKEZA KWA KUKOSA ELIMU HIYO

ELIMU KWA UMMA JUU YA HIFADHI YA MAZINGIRA INAHITAJIKA KATIKA JAMII ZINAZOISHI NA KUJISHUGULISHA PEMBEZONI MWA MILIMA YA ASILI ILI KUEPUKA UALIBIFU UNAOJITOKEZA KWA KUKOSA ELIMU HIYO C:\Documents and Settings\Administrator\My Documents\DCIM\127___03\IMG_4423.JPG
PICHA JUU: Mlima ukiungua moto katika kijiji cha Nyakunguru ambao chanzo chake  kilijulikana na
                    lengo ni kuuanda mlima ili kuchipua nyasi mpya kwa ajili ya malisho ya ng’ombe na ukataji   
                    kuni.

Elimu kwa umma juu ya hifadhi ya mazingira ni vyema kutolewa katika jamii ya Kitanzania kwani jamii nyingi hazijui mathara yanayoweza kutokea kwa uchomaji ovyo uoto wa Asili uliopo kwenye mabonde na Milima.
Uharibifu huu utokanao na uchomaji moto uoto wa Asili  ndio unaopelekea maeneo mengi katika nchi ya Tanzania kukumbwa na adha itokanayo na mabadiliko ya Tabianchi ambayo chanzo chake ni uaribifu wa mazingira , na hii inajidhihilisha wazi kutokana na vilio na matukio makubwa yanayoikumba nchi yetu ya Tanzania, mfano wakulima utawasikia wakilalama juu ya kubadilika badilika kwa misimu ya mvua, ukame, mvua kupita kiasi inayosababisha mafuliko ikiwa ni pamoja na joto kali.

Serikali inalojukumu la kuchukua hatua ya kuandaa sera na kutunga sheria itakayosimamia matumizi ya moto ili kupunguza uharibifu wa mazingira.

Shirika la Taeca kupitia wanachama wake wameandaa mpango wa mwaka mzima wa kutoa semina ya elimu ya mazingira katika shule za msingi na sekondari katika wilaya ya Tarime, na hili zoezi litaambatana na kuandaa vipepelushi vyenye mafunzo rahisi ya hifadhi ya mazingira na kuvigawa kwa wananchi kama njia rahisi ya kueneza elimu hii ya utunzaji wa mazingira.


C:\Documents and Settings\Administrator\My Documents\DCIM\127___03\IMG_4480.JPG
PICHA JUU: Mlima   Nyarero Wilaya Tarime baada ya kuteketea kwa moto ambao haukujulikana  chanzo      chake.










About TAECA.TZ

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment