SHIRIKA LA TAECA LATUNUKIWA TUZO KWA KUBORESHA MAZINGIRA YA SHULE YA SEKONDARI NYAMWAGA –TARIME VIJIJI.



shirika la  TAECA limefanikiwa kutunukiwa cheti kwa ushiriki wake katika uboreshaji wa mazingira, wanachama wa shirika la TAECA wanayo juhudi na kiu kubwa sana kufikia malengo yao ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya Nchi yanayozikumba nchi nyingi Duniani hususani nchi zinazoendelea kwa kuleta madhara makubwa kama vile ukame, mvua nyingi zinazoleta madhara, kuongezeka kwa joto duniani.
Shirika la TAECA Pamoja na jitahada zote hizo linakabiliwa na changamoto nyingi sana zikiwemo fedha za kuendesha shirika kwani hadi sasa shirika halijapata ufadhili wowote unaoweza kusaidia shirika kufanikisha malengo yake, nah ii imesababisha shirika la TAECA kufanya shughuli zake ndani ya wilaya ya Tarime tu na kushindwa kugharamia  gharama za kutoa huduma katika maeneo mengine katika Tanzania Bara kwa mujibu wa usajili wa shirika.
Hivyo basi shirika linawaoba wadau wengine wa mazingira ikiwamo Serikali ya Tanzania na wafadhili mbalimbali waweze kulisaidia shirika kifedha na kielimu ili liweze kufanikisha malengo yake ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.






About TAECA.TZ

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment