Shule ya Sekondari J.K. NYERERE ni miongoni mwa shule mpya zilizojengwa kwa makubaliano yaliyofikiwa kati ya kijiji cha Nyamwaga na kampuni ya uchimbaji dhahabu ya ACACIA North Mara, shule hiyo iliyowekwa jina la msingi na Mke wa Hayati Baba wa Taifa la Tanzania Mama Maria Julius Kambarage Nyerere, kwa sasa ina kidato cha kwanza na cha pili na walimu wenye uzoefu mkubwa katika Nyanja ya ufundishaji wa masomo ya Sayansi na arts, inatarajia kuwa na kidato cha kwanza hadi cha sita baada ya kukamilika kwa ujenzi wa shule hiyo yenye vyumba vya madarasa, maabara na nyumba za walimu za kisasa kabisa, kwakweli miundombinu ya shule hii ni ya aina yake kabisa kiasi kwamba ni shule inayotarajiwa kuwa mkombozi wa watoto wa vijiji vilivyopo jirani na shule hiyo kwa kutoa watoto wazuri katika masomo ya sayansi.
Shirika la TAECA kwa kushirikiana na uongozi wa shule hiyo wameamua kuboresha mazingira ya shule hiyo kwa kupanda miti ya aina mbalimbali ili yaendane na mandhali ya majengo yaliyopo ili shule hiyo imuenzi mwasisi wa Taifa la Tanzania Mwl Julius Kambarage Nyerere kwa Majengo mazuri, Taaluma bora na ya hali ya juu ikiwa ni pamoja na mazingira yenye kumvutia mwanafunzi katika kujifunza kwake.
0 comments :
Post a Comment